We Are Celebrating 60 years (Diamond) Jubilee!
Monday - Sunday, 24 hrs
Call us now +255 685 487 936

Tangazo la Nafasi za Ajira

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA
Hospitali ya Wasso - Jimbo Kuu Katoliki Arusha

Wilaya ya Ngorongoro


HOSPITALI YA WASSO - JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA

WILAYA YA NGORONGORO

Hospitali ya Wasso ni hospitali ya kanisa jimbo kuu katoliki la Arusha inayotoa huduma za afya kwa jamii ya Ngorongoro na maeneo ya jirani.

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wasso anakaribisha maombi ya kazi kwa kada ya Afisa Hesabu Daraja la II.

1. AFISA HESABU DARAJA LA II (ACCOUNTS OFFICER II) NAFASI (1)

a)  SIFA ZA MWOMBAJI

•   Awe na Shahada ya Uhasibu, Fedha, Uchumi au fani inayohusiana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali

•   Awe mwenye CPA (T) au sifa nyingine inayolingana na kutambuliwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).

•   Awe amesajiliwa na NBAA kama Certified public Accountant.

•   Awe na ufahamu wa mifumo ya kifedha ya Serikali na Mifumo mingine ya Kiteknolojia ya uhasibu

•   Awe na uwezo mzuri wa kutumia kompyuta, hasa programu za uhasibu na MS Office (Word, Excel, Outlook).

•   Awe na uzoefu au uelewa wa masuala ya fedha katika Sekta ya Afya.

•   Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa umakini, uadilifu, uaminifu na kwa kufuata taratibu za kifedha.

•   Awe na mawasiliano mazuri, nidhamu, na uwezo wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine.

b) MAJUKUMU YA KAZI

•    Kuandaa na kutunza kumbukumbu za fedha za Hospitali kwa mujibu wa kanuni na taratibu.

•    Kuhakikisha Mapato na Matumizi yote ya fedha yanarekodiwa ipasavyo kwenye mifumo ya uhasibu.

•    Kuandaa hatimiliki. Vocha, Risiti, Malipo na nyaraka zote za kifedha.

•    Kufanya upatanisho wa akaunti (Bank Reconciliation) kila mwezi.

•    Kushiriki katika kuandaa bajeti ya mwaka, tathmim ya bajeti na taarifa za fedha za robo mwaka na mwaka mzima.

•    Kuandaa na kuwasilisha taarifa za kifedha kwa uongozi wa Hospitali.

•    Kufanya uhakiki'wa madai kabla ya kufanyika kwa malipo.

•    Kushiriki katika ukusanyaji na ufuatiliaji wa mapato ya Hospitali

Deadline: 31st December 2025

Biomedical Engineer grade II
Hospitali ya Wasso - Jimbo Kuu Katoliki Arusha

Wilaya ya Ngorongoro


Mhandisi wa Vifaa Tiba daraja la II (Biomedical Engineer grade II) NAFASI(1) a) SIFA ZA MWOMBAJI • Awe na cheti cha kidato cha nne au kidato cha sita, stashahada au shahada ya Sayansi ya uhandisi wa vifaa Tiba (Biomedical Engineering) kutoka chuo kinachotambulika na NACTE • Awe na ujuzi wa kutumia na kutengeneza vifaa vya kitabibu vya kielektroniki na vya umeme. • Awe na uelewa wa msingi wa kompyuta na program zinazotumika katika ufuatiliaji wa vifaa vya tiba. • Uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yoyote. • Awe tayari kufanya kazi kwa muda wa ziada au kufika kazini haraka endapo kutatokea dharura ya kifaa muhimu kuharibika. b) MAJUKUMU YA KAZI • Kufanya matengenezo ya mara kwa mara na ukarabati wa vifaa vya tiba vya hospitali ili viwe katika hali nzuri ya kufanya kazi muda wote. • Kuimika (install) na kujaribu (test) vifaa vipya vya tiba vinavyowasili hospitalini kan=bla ya kuanza kutumika. • Kutunza kumbukumbu za vifaa vya tiba, ikiwemo tarehe za matengenezo na hali ya kifaa. • Kushirikiana na wauguzi na madaktari kuhakikisha vifaa vinatumiwa ipasavyo na kwa usalama. • Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu ununuzi, matumizi, na uboreshaji wa vifaa vya tiba vipya. • Kuhakikisha kanuni na miongozo ya usalama wa vifaa vya umeme na vya kitabibu inazingatiwa. • Kutayarisha ripoti za matengenezo, ukaguzi wa vifaa, na mapendekezo ya bajeti ya vifaa vya kitabibu. • Kufanya mafunzo mafupi (orientation) kwa watumishi wanaotumia vifaa vya tiba vipya.

Deadline: 30th November 2025

MPISHI DARAJA LA II (COOK GRADE II) NAFASI (1)
Hospitali ya Wasso - Jimbo Kuu Katoliki Arusha

Wilaya ya Ngorongoro


1. MPISHI DARAJA LA II (COOK GRADE II) NAFASI (1) a) SIFA ZA MWOMBAJI • Awe na cheti cha kidato cha nne au kidato cha sita. • Awe na Cheti cha Hotel Management kutoka chuo kinachotambulika na Serikali. • Awe na uzoefu wa angalau miaka miwili (2) katika Hoteli, Lodge au hosteli ya kitalii. • Uwezo wa kuandaa vyakula vya kimataifa (Continental & African dishes) utapewa kipaumbele. • Awe na uelewa wa masuala ya usafi wa chakula, huduma kwa wateja (Customer care), na usalama wa chakula (Food safety standards). Awe na maadili mazuri, Mwaminifu, mchapakazi, na mwenye uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu kulingana na ratiba ya wageni b) MAJUKUMU YA KAZI • Kupika na kuandaa chakula bora kwa wageni na watalii wanaofikia katika Hospitali yetu kwa kuzingatia viwango vyenye ubora. • Kuandaa menyu mbalimbali (Local & continental dishes) kulingana na mahitaji ya wageni. • Kuhakikisha sehemu ya jikoni, vyombo na vifaa vya upishi vinakuwa safi muda wote. • Kusimamia upokeaji, uhifadhi na matumizi sahihi ya malighafi za chakula. • Kuhakikisha huduma za chakula zinatolewa kwa wakati, kwa usafi na kwa ukarimu. • Kushirikiana na Uongozi katika kuboresha huduma na kuridhisha wateja. • Kuhakikisha gharama za upishi zinadhibitiwa na kuzingatia bajeti ya mapato ya hostel.

Deadline: 30th November 2025